Zuwia meno kuoza
Kuoza meno ni ugonjwa wa meno unaosababishwa na asidi inayozalishwa na bacteria wanaoishi mdomoni( normal flora). Asidi hii huondoa madini kama calcium ambayo huimarisha meno na mifupa.
Ili bacteria waweze kusababisha uzalishaji wa asidi kwa wingi inayoweza kupelekea meno kuoza, kinahitajika chakula cha sukari ambacho ndicho hubadilishwa na bacteria hao kuwa asidi inayopelekea meno kuoza.
Sio kila chakula cha sukali hupelekea meno kuoza, isipokua vyakula vya sukari vinavyo zalishwa viwandani (cariogenic foods) kama vile soda, pipi, chokleti, sukari nk.
Vyakula vya asili na vyenye sukari kama vile viazi vitam, ndizi mbivu, nanasi, muwa nk, haviwezi kusababisha meno kuoza.
Kwakadiri miaka inavoendelea na utandawazi kuongezeka ndivyo watu wanaachana na vyakula asili, hili hutoa jibu kwanini miaka ya sasa tatizo hili linaongezeka ukilinganisha na zamani.
Mambo yanayo pelekea meno kuoza
1. SukariMatumizi ya sukari Mara kwa mara husababisha uzarishwaji wa asidi kwa wingi inayopelekea meno kuoza.
Hoja sio uwingi wa sukari ila idadi ya matumizi kwa siku (frequency). Je, vyakula hivi hutumiwa marangapi kwa siku? ongezeko la matumizi huhatarisha meno kuoza hatakama unapiga mswaki.
2. Bacteria
Aina ya bacteria waliopo mdomoni na ukuaji wake (ongezeko lake) hupelekea ongezeko la uzalishaji wa asidi hatari kwa meno.
Bacteria huongezeka zaidi pale kinywa kinapo kuwa kichafu chenye mabaki mengi ya chakula ya muda mrefu ambayo hubadilishwa na kuwa ugaga(vitu vigumu vilivyo ganda juu ya meno). Vitu hivi hutengeneza makazi mazuri ya bacteria.
3. Meno yenyewe
Kuoza kwa meno hutegemeana na hali ya mwili ya mtu binafi kuweza kupambana dhidi ya tatizo. Hivyo wapo watu ambao kinga ya meno yao dhidi ya kuoza ni kubwa zaidi ya wengine.
4. Muda
Meno huchukua muda mrefu mpaka kufikia yanaoza ukayagundua, sio jambo la siku chache bali ni la miezi kadhaa hadi miaka.
Matokeo ya baadae ya kuoza meno
Jino kuuma au kuhisi ganzi linapopitiwa na vitu vya baridi na moto au vyenye sukari.kupoteza jino, jino kung'olewa endapo limelika sana au pale linaposababisha magonjwa mengine mdomoni.
Majipu ya mdomoni yanaweza kusababishwa na meno kuoza hasa pale bacteria wanapo pata nafasi ya maambukizi.
Maambukizi ya mfupa wa taya (ostemylitis), hili linaweza kupelekea kukatwa sehemu au kuondoa taya lote.
Kifo, mtu akipata magonjwa kama majipu makubwa, Kansa au maambukiza katika misuli ya usoni, anaweza kupoteza maisha.
Namna ya kuzuwia
Ili kuzuwia meno kuoza inapasa kupunguza utumiaji wa sukari mara kwa mara, utumiaji usizidi mara tatu kwa siku.Piga mswaki walau mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kabla ya kulala yaani baada ya chakula cha usiku. Jifunze namna ya kupiga mswaki kwa usahihi ili kuhakikisha kinywa chote kinawekwa safi.
Sukutua kinywa chako kila baada ya kutumia vyakula vya sukali vizalishwavyo viwandani kama vile pipi.
Epuka kulala usingizi na vyajula hivi mdomoni, hakikisha pia mtoto halali na vyakula hivi mdomoni.
Tembelea mara kwa mara kliniki ya meno walau mara mbili kwa mwaka ili kuchunguza kama kunadalili ya kuoza meno. Hili itakusaidia kujua na kukinga matatizo mengine ya kinywa na mano.
Tumia dawa ya meno wakati wa kupiga mswaki, hakikisha dawa unayotumiwa ina fluoride. Flouride husaidia kurudisha madini katika meno.
Nenda kliniki ya meno endapo una meno yaliyooza ili uyazibe kwa dawa yasindelee kuoza. Watu wengi kuenda kliniki baada ya maumivu jambo ambalo hupelekea jino kung'olewa.
Usikubali kupoteza jino lako hata moja kwani linakazi yake muhimu.
Fuatana nami katika blog yangu au piga simu:
+255752674467
+255676674467
Maada zinazo fanana
Afya ya uzazi na mahusiano
Afya ya mama na matoto
Afya ya mwili na akili nk
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni