Ijumaa, 10 Februari 2017

kutokwa harufu mbaya ukeni

Sababu za kutokwa harufu mbaya ukeni



    Tatazo hili limekuwa likiwakabili baadhi ya wawake na wengi  wao wamekuwa wakitafuta suruhisho lakini wakakosa.

    Kutokwa harufu ukeni ni jambo ambalo linaweza kupunguza nguvu ya upendo katika mahusiano ya kimapenzi ya wana ndoa. Kwakuwa harufu inaweza sikika zaidi wakati na baada ya tendo la ndoa, mwanaume anaweza kushindwa kuivumilia na kutokuwa na hamasa ya kufanya tendo hilo.

   Baadhi ya wanawake wamekuwa wakidhani harufu haipasi kutoka katika uke hilo sio sahihi, isipokua kama sehemu nyingine za viungo uke pia unatoa harufu ambayo ni yakawaida isiyo ambatana na dalili zozote za kuashiria ugonjwa.

    Harufu kidogo inaweza kutoka hasa baada ya kutoka hedhi na baada ya tendo la ndoa pale mbegu za kiume zinapo kutana na uke na kubadili hali ya asidi-basi yake, na hili linaweza kuwa la kawaida na hutokea kutegemeana na mwanamke.

   Tatizo huwa pale ambapo harufu inakuwa kali zaidi au pale harufu inapoendelea kwa siku nyingi baada ya kutoka hedhi, hili huashiria maambukizi ya ugonjwa au sababu nyingine tutakazo ziangalia.

   Tutangalia sababu ya tatizo hili na namna ya kutibu.
 
   Sababu zinazo pelekea tatizo

1.  Kutokuwa msafi wa mwili
   Kama ilivyo kawaida kwa ngozi kutoa harufu pale jasho linapo mtoka mtu, pia mtu asiye msafi hasa katika sekemu za nje za uke anaweza kutoa harufu mbaya, na husikika hasa wakati wa tendo la ndoa na baada ya kazi.

    Hili ni kutokana na kuwepo kwa tezi zinazotoa kemikali kama vile zitoavyo za sehemu nyingine kama kwapa.

2. Maambukizi
    Harufu inapokuwa mbaya na kali na wakati mwingine kama harufu ya samaki, huwa ni kwasababu ya maambukizi.

    Harufu huambatana na muwasho au maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa na wakati wa kukojoa.

    Yapo magonjwa ya sehemu za uke yanayo sababisha harufu na yanasababishwa na baadhi ya protozoa, fangasi na bacteria.

3. Mabadiliko ya homoni mwilini

   Katika nyakati mbalimbali ndani ya mzunguko wa hedhi, hutokea mabadiliko aina mbalimbali ya homoni. Wakati ambao harufu inaweza kuongezaks ni ule ambao homono aina ya oestrogeni inapokuwa imepungua mwilini mwa mwanamke hasa zile siku zinazokamilisha mzunguko wa hedhi. Wastani wasiku Kumi kabla ya kuingia hedhi.

4. Chakula unachokula

   Vipo aina ya vyakula ambavyo huwa na harufu kali kama vitunguu swaumu, samaki, kabeji nk. Utafiti unaonesha kuwa vyakula hivi vinapotumiwa husababisha harufu ya ngozi na uke kuongezeka.

5. Kusaulika au kuachwa kwa pedi kwa muda mrefu
   Kuachwa kwa pedi muda mrefu kunaweza kusababisha ongezeko la ukuaji wa bacteria, jambo hili pia linaweza kuzalisha harufu mbaya.

6. Kutawadha uke kwa maji.

   Kusafisha sana uke mara kwa Mara huondoa aina ya bacteria wasio dhuru ambao huhakikisha wanailinda sehemu ya uke dhidi ya maambukizi na magonjwa.

   Inapasa kusafisha katika sehemu za nje za uke wakati wa kuoga pia baada ya haja ndogo ili kuweka sehemu hizo kuwa safi.

Namna ya kukinga

Ili kukinga tatizo hili, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:

    Kuhakikisha hali ya usafi wa mwili na sehemu za siri.

   Badili nguo hasa za ndani baada ya mazoezi au kazi.

   Vaa nguo za ndani nyepesi, zisizo bana na za matilio ya pamba (cotton).
    Usijitawadhe ndani ya uke.
  Punguza unene na uzito endapo unahisi ni chanzo cha kutoa jasho mara kwa Mara.

Tiba ya tatizo

    Ikiwa unatokwa usaha, unahisi muwasho na harufu mbaya ukeni, nenda hospitality au kituo cha afya kilicho kari nawe umwone daktari hili afanye uchunguzi madhubu na kukupatia matibabu. Matibabu yapo kutegemeana na aina ya vimelea walisababisha ugonjwa huo.

   Hizi dalili huja endapo umepata maambukizi, na maambukizi hayo hupona haraka yakiwahiwa kwa matibabu.

Endelea kufuatana nami katika maada za afya katika makala zangu katika blog yangu, au piga simu :
+255752674467 au
+255676674467

Maada zinazo fanana
Afya ya mama na mtoto
Aya ya kinywa na meno
Afya ya mwili na akili nk

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni