Alhamisi, 30 Machi 2017

Jua sababu zinazozuwia mwanamke kushika ujauzito

Unazijua sababu zinazopelekea mimba kushindwa kutunga?

     Wapo watu wanao dumu katika ndoa zao kwa miaka mingi bila kupata mtoto. Watu wingi huwa wepesi kuwatupia wake zao lawama kwakudhani kuwa wao tu ndo chanzo.

   Hapa tutaangalia sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kushindwa kushika ujauzito zinazosababishwa na mwanamke na mwanaume kama ifuatavyo;

1. Uzito

     Mwanamke mwenye uzito mkubwa 15% zaidi ya anavopasa kuwa nao huweza kupunguza uwezekano wa yeye kushika ujauzito.

     Pia alie na uzito mdogo 15% ya anavopasa kuwa inaweza kupunguza uwezekano wa kushika ujauzito.

2. Kubadilika kwa mpangilio sahihi wa homoni kwa mwanamke


     Kubadilika kwa mpangilio huo husababisha kuwa na mzunguko wa hedhi ndefu au fupi na huweza badilika badilika.  Kutokana na hilo mwezi mpevu huathiliwa.

3. Matumizi ya madawa


     Matumizi ya dawa za maumivu na za magonjwa ya muda ndefu inaweza kuzuwia mwanamke kushika ujauzito kwa kipindi fulani.

4. Matumizi ya tumbaku na pombe


      Matumizi ya vitu hivo vinaweza kupunguza uwezekano wa mwanamke kupata mimba.   Pia inaweza kusababisha mwanaume kusindwa kusababisha ujauzito kwa mwanamke.

5. Magonjwa ya mirija ya folopi na mji wa mimba.


     Magonjwa haya husababisha makovu katika mji wa mimba na na kufanya yai lililorutubishwa kutoweza kutungwa.

   Pia huweza kusababisha kuziba kwa mirija hiyo na kupelekea kuzuwia urutubishaji.
  Maranyingi magonjwa haya huwa ya zinaa ingawa kansa ya uzazi na ovari husababisha utasa pia.

6. Mwanaume wenye historia ya magonjwa kama tezi dume na maambukizi katika via vya uzazi pia yanaweza kupunguza uwezekano wa kusababisha mimba.
Add caption