Ijumaa, 30 Juni 2017

Rudisha nguvu za kiume zilizopotea

Namna ya kurudisha nguvu za kiume zilizopotea kwasababu ya kuongezeka unene

    Kupoteza au kupungukiwa nguvu za kiume ni hali ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume, uume kusimama kilegevu, kupoteza hamu ya tendo la ndoa baada ya kufika kileleni Mara moja, uume kushindwa kusimama hadi unapofika kileleni au kukosa hamu ya kufanya tendon la ndoa. Hali hii huwapata wanaume wengi wa rika zote ingawa ni tatizo zaidi kwa wanaume walio na umri wa miaka 50 na kuendelea.

    Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume, hapa tutaangalia tatizo la unene linavyoweza kusababisha tatizo na namna ya kulitibu.
   Unene huweza kupelekea matatizo ya msukumo wa damu ambayo hufanya kupungua kwa kiwango cha damu inayojaa katika misuli ya uume, jambo hili huweza kupelekea nguvu za kiume kupungua au kuimengi
 

 Namna ya kutibu tatizo

   Ili kurejesha nguvu zako za kiume unapasa kufanya yafuatayo
Fanya jitihada za kupunguza unene na uzito wako uliozidi. Zipo njia mbalimbali za kupunguza unene ikiwepo kufanya mazoezi yakutosha, kutengeneza aina ya mlo utakaopunguza unene ndani ya muda mfupi pamoja na nyinginezo. Yako masomo mengine yanayo kufundisha namna ya kufanya ili kupunguza unene.
Kunywa maji mengi na kula matikitiki maji kwa wingi ili kusafisha mfumo wa mzunguko wa damu.

Kula matunda na mboga za majani kwa wingi kuliko vyakula vya nyama na wanga.
Kula kwa wingi vyakula kama mbegu za maboga, karanga, nazi na jamii zake.
Tumia vitunguu swaumu marambili kwa Siku, chukua vipande sita hadi nane vya kitunguu swaumu, vimenye kisha uvikatekate katika vipande vidogovidogo kisha uvinywe kama vidonge, Fanya zoezi hilo kwa mwezi mmoja.


 

Jumatano, 3 Mei 2017

Yajue magonjwa ya fangasi ya ngozi na matibabu yake

Magonjwa ya fangasi ya ngozi na matibabu yake

      Fangasi ni magonjwa yanayoathiri ngozi, kucha na nywele, pia huathiri mdomoni na ukeni. Magonjwa haya huambukiza kwa njia ya kugusana ua kshirikiana nguo hasa za ndani na tauro.

      Hapa tutaangalia fangasi katika kundi la magonjwa yanayoathiri ngozi, nywele na kucha (dermatomycosis).

      Kuna aina kuu 5 za magonjwa ya fangasi wa ngozi, nywele na kucha kama ifuatavyo;


  • Fangasi wa kichwani, ugonjwa huu huanza na sehemu ndogo ya ngozi ya kichwa na kukua kuwa sehemu kubwa. Huathiri nywele na kuzifanya dhaifu, laini na nyepesi kukatika au kung'oka. Huwaathiri sana watoti chini ya miaka 10 na hupotea mtu akisha barehe. Matibabu take  ni  griseofulvin na fluconazole, dozi zake huanzia siku 6-14.



  • Fangasi wa mwili, ugonjwa huu hutokea mwilini, sehemu ya ngozi iliyoathiriwa huwa nyekundu, duara kama shiringi na kukua huku ikiacha sehemu ya katikati kuwa na ngozi nzuri. Maduara haya yanaweza kukaa yakiwa kadhaa katika sehemu moja ya ngozi. Dawa nzuri kutumia ni za kupaka zinazokuwa katika tyubu, cotrimazole au ketoconazole. Kwa ugonjwa uliokua sana na kwa wagonjwa wenye kinga ya mwili ndogo kama wenye VVU, nivema wakatumia dawa ya kunywa




  • Fangasi wa nyayo na vidole, ugonjwa huu hutokea kama mabaka na kuchanika katikati ya vidole na huwacha sana na kuuma pia. Matibabu yake maranyingi huwa dawa ya kupaka kwa wiki 4, kwa ugonjwa uliokua sana tumia dawa ya kunywa kama griseofulvin kwa wiki 6-12.



  • Fangasi wa kucha, ugonjwa huu huathiri kucha na hubadilisha rangi ya kucha. Huzalishwa vitu kama chaki na ambavyo vikisuguliwa huweza kupukutika. Kucha huweza kulika na inaweza kuisha. Ili kutibu ugonjwa huu nibora kutumia dawa za kunjwa na terbinafine na itraconazole zimeonekana dawa bora zaidi.



  • Pityriasis, huu ni ugonjwa wa fangasi ambao huathiri sehemu ya huu sana ya ngozi katika sehemu za usoni, shingoni na mgongoni. Hutokea kama viduara vyenye mng'ao vinavyo washa. Huongezeka na huathiri sehemu kubwa ya ngozi visipotibiwa ingwa vinaweza kupotea vyenyewe. Maranyingi ugonjwa huu hauambukizwi Ila hutokea kama ajari tu yaapotikea mabadiliko fulani ya mwili. Sio ugonjwa hari sana kiafya ila haukubaliki kwani huharibu mwonekano wa mtu has a unapotokea maeneo ya uso na shingoni. Matibabu yake ni sawa na yale ya fangasi wa mwili.

Jumamosi, 29 Aprili 2017

Jua ugonjwa wa kuoza fizi na namna ya kuuzuwia na kuutibu

Ugonjwa wa kuoza fizi

   Ugonjwa wa kuoza fizi ni ugonjwa unaotokea Mara chache na hutokea zaidi katika nchi zinazoendelea Kama Tanzania hasa katika maeneo ya watu maskini. Ugonjwa huwa hatari ikiwa utaendelea sana na kusababisha fizi kuozasana has a pale unapopelekea maambukizi ya magonjwa mengine.

Mambo yanayoweza kupelekea  ugonjwa huu

  • Kinywa kichafu, uchafu wa kinywa hupelekea kukua kwa bacteria hatari wanaoweza kupelekea ugonjwa.
  • Uvutaji sigara na matumizi ya ugoro na kubeli yanaweza kupelekea tatizo.
  • Afya mgogoro, mtu mwenye afya mgogoro anaweza kupelekea bacteria walio kinywani wasio na madhara kupelekea madhara na kusababisha ugonjwa.
  • Msongo wa mawazo
  • Kinga ya mwili kushuka kutokana sababu mbalimbali ukiwemo UKIMWI au magonjwa sugu kama kisukari.
  • Maambukizi ya magonjwa ya kinywa

Dalili za ugonjwa

Harufu mbaya ya kutoka kinywani na kuhisi radha mbaya
  • Damu kuvuja katika fizi kwa urahisi
  • Vidonda katika fizi
  • Kuvimba fizi na kuwa njekundu
  • Fizi kuuma
  • Fizi koza na kupukutika
  • Fizi kutokwa usaha

Matibabu 

Unapoona dalili za namna hii hapo juu, nivema uende hospitality ili ukaonane na daktari wa kinywa na meno, ikiwa unashindwa kuhospitali, fanya yafuatayo
  • Safisha kinywa chako kwa maji na kitambaa safi na laini
  • Nunua dawa ya kusukutua kinywani ( chlorhexidine ), sukutua kinywa chako kwa kufuata maelekezo utakayopewa unapoinunua.
  • Tumia amoxicycilne na paracetamol endapo unahisi msumivu ya fizi au homa, unaweza kiongeza metronidazole (frajiri) endapo tatizo ni kubwa. Tumia dozi ya Sikh tank kwa hili dawa isipokuwa paracetamol ambayo unaweza kutumia kwa Siku 3, hakikisha unafuata maelekezo ya matumizi ya dawa hizo uliyopewa wakati unazinunua.

Namna ya kukinga ugonjwa

Hakikisha unafanya usafi wa kinywa chako na kutembelea kliniki ya kinywa na meno walau Mara 2 kwa mwaka ili kupata ushauri, kukinga na kutibu magonjwa nyemerezi ya kinywa na meno.


Jumamosi, 22 Aprili 2017

Jua namna ya kumsaidia mtu aliepata mshituko

Ujue mshituko na namna ya kumsaidia mtu aliyepatwa na mshituko (Shock)


      Mshituko ni tatizo la kiafya linalompata mtu kutokana na kupungua kwa damu katika ubongo au kuathiliwa kwa mfumo wa fahamu. Tatizo hili linaweza kumpata mtu wa jinsia yoyote na umri wowote.

      Zipo aina tano za mshituko kama ifuatavyo;

  •   Mshituko unaosababishwa na  matatizo ya moyo
  • Mshituko unaoshababishwa na upungufu wa damu
  • Mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu 
  • Mshituko unaosababishwa na aleji
  • Mshituko unaosababishwa na kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu


   Mshituko unaosababishwa na moyo

       Moyo unaweza kushindwa kusukuma damu katika baadhi ya viungo kama ubongo na kupelekea kupungua kwa oksijeni katika ubongo, jambo hili linaweza kupelekea mshituko.
Moyo unaweza kushindwa kusukuma damu ipasavyo kutokana na magonjwa ya moyo.

Mshituko unaosababishwa na kupungua kwa damu

      Kupungua kwa damu katika mzunguko wake hupelekea kupungua
kwa kiwango cha damu inayosukumwa kuenda katika ubongo na kupelekea mshituko.
       Kupungua kwa damu katika mzunguko wake kunaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;

  • Kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi
  • Kuungua
  • Kuharisha
  • Maji kukimbilia sehemu za wazi za mwili kama zile zinazozunguka mapafu na tumbo

Mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu

      Hii hutokea pale bacteria wanapoingia katika damu na kumsikumo sumu. Sumu hii inapokua katika damu husababisha kulegea na kutanuka kwa mishipa ya damu. Mishipa ikitanuka hupunguza msukumo wa damu na kupelekea damu kushindwa kufika sehemu za juu za mwili hasa katika ubongo, jambo hili huweza kusababisha mshituko.

Mshituko unaosababishwa na aleji

      Hii hutokea pale chemikali toka nje ya mwili zinaposhindana na mwili na kusababisha kulegea na kutanuka kwa mishipa ya damu. Hali hii kupelekea kupungua msukumo wa damu na kufanya upungufu wa damu kufika katika ubongo na kupelekea mshituko.

Mshituko unaosababishwa na kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu

      Hii hutokea pale mtu anapopata msongo wa mawazo au uwoga, mfumo wa fahamu huweza kuathirika na kupelekea mshituko.

Dalili za mshituko


  • Ngozi baridi iliyopauka isipokuwa kwa mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu ambayo ngozi huwa yenye joto
  • Kuchanganyikiwa akili na kukosa utulivu
  • Kutokwa na jasho
  • Kutokupata mkojo
  • Kubadilika rangi na kuwa mweupe rangi inanyoonesha upungufu wa damu
  • Mgonjwa anaweza kupoteza fahamu
  • Pumzi ya chini na ya harakaharaka na mapigo ya moyo kuwa ya harakaharaka


Namna ya kumsaidia mgonjwa


  • Mweke mgonjwa katika sehemu yenye hewa safi na yakutosha
  • Regeza nguo za mwili wake
  • Mlaze mgonjwa chali na kichwa chake kikitazama upande kuruhusu mate kutokana nje ili asipakiwe, hii ni kwa mgonjwa alipoteza fahamu
  • Mlaze miguu yake ikiwa juu kidogo kichwa kikiwa chini kidogo kuruhusu damu kushuka katika ubongo
  • Akiwa katika hali nafuu apelekwe hospitali haraka ambako atapewa matibabu ikiwa ni pamoja na kuongezewa maji au damu na kupewa dawa.
  • Ikiwa mgonjwa amepata mshituko kwasababu ya kuvuja damu nyingi, inapasa kwanza kuzuwia damu kuvuja kisha huduma zingine zifuate ikiwa ni pamoja na kumuwahisha hospitali




Jumatatu, 3 Aprili 2017

Madhara ya utando mgumu katika meno

Jua madhara ya utando mgumu kwenye meno (calculus)


     Utando mgumu kwenye meno kwa jina la kitaalamu huitwa calculus,  utando huu huwa mgumu kiasi kwamba hauwezi kutoka kirahisi. Huwa na rangi tofauti tofauti kuanzia njano hadi nyeusi kutokana na hatua ya ukuaji wake.



     Calculus hutokea baada ya mabaki ya chakula yenye bacteria kwa wingi kukaa kwa muda ndefu hadi miezi kadhaa.

Madhara ya calculus 


1. Memo kuoza


     Utando huu huweka makazi mazuri kwa bacteria ambao hupelekea meno kuoza. Pia huweza kupelekea mabaki ya chakula kuongezeka na kuwawezesha hawa bacteria kujipatia chakula na makazi mazuri. Shughuli za bacteria hawa hupelekea jino kuoza katika eneo hilo.

      Kuoza meno kunaathari kubwa kiafya kwani kunaweza kupelekea kupoteza meno na magonjwa makubwa hata kupoteza maisha.

2. Fizi kushuka chini na kuacha mzizi wa jino wazi


   Calculus hupelekea fizi kushuka chini na kuacha mzizi wa jino wazi,  hii inaweza kupelekea kuhisi ganzi au maumivu ya jino kutokana na mzizi kuachwa wazi. Pia inaweza kupelekea jino kulegea na kufikia hata ya kung'olewa.


  3. Magonjwa ya fizi


     Calculus inaweza kupelekea magonjwa ya fizi kama gingivitis na periodontitis.   Gingivitis ni ugonjwa ambao hupelekea fizi kuvimba na kutokwa damu zinapo guswa kidogo.

     Periodontitis ni magonjwa ya fizi na mifupa ya taya, huambatana na fizi kuvuja damu, kuvimba,  kuoza na kutoa usaha. Pia hupeleke kulika kwa mfupa wa taya na kufanya meno kulegea.


4. Kusababisha magonjwa ya moyo


     Maambukizi ya bacteria huweza kupenya na kuingia katika mfumo wa mzunguko wa damu. Hii huweza kusababisha magonjwa ya moyo na dumu katika damu.
Namna ya kuzuwia calculus

     Ili kuzuwia utando huu,  hakikisha unapiga mswaki wako vizuri namna inayoruhusu pande zote za meno zinakuwa safi. Jifunze namna ya kupiga mswaki ili kuhakikisha usalama wa kinywa chako.


     Tembelea hospitali katika kliniki ya kinywa na meno ili utando huu uondolewe.   Ikiwa utando huu umeleta madhara katika afya yako, hakikisha utando huu unatolewa na matibabu yanatolewa ili kuzuwia ukuaji na madhara tatizo yanayoweza kujitokeza.
 

Kwamawasiliano piga; 
+255752674467
+255676674467

Alhamisi, 30 Machi 2017

Jua sababu zinazozuwia mwanamke kushika ujauzito

Unazijua sababu zinazopelekea mimba kushindwa kutunga?

     Wapo watu wanao dumu katika ndoa zao kwa miaka mingi bila kupata mtoto. Watu wingi huwa wepesi kuwatupia wake zao lawama kwakudhani kuwa wao tu ndo chanzo.

   Hapa tutaangalia sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kushindwa kushika ujauzito zinazosababishwa na mwanamke na mwanaume kama ifuatavyo;

1. Uzito

     Mwanamke mwenye uzito mkubwa 15% zaidi ya anavopasa kuwa nao huweza kupunguza uwezekano wa yeye kushika ujauzito.

     Pia alie na uzito mdogo 15% ya anavopasa kuwa inaweza kupunguza uwezekano wa kushika ujauzito.

2. Kubadilika kwa mpangilio sahihi wa homoni kwa mwanamke


     Kubadilika kwa mpangilio huo husababisha kuwa na mzunguko wa hedhi ndefu au fupi na huweza badilika badilika.  Kutokana na hilo mwezi mpevu huathiliwa.

3. Matumizi ya madawa


     Matumizi ya dawa za maumivu na za magonjwa ya muda ndefu inaweza kuzuwia mwanamke kushika ujauzito kwa kipindi fulani.

4. Matumizi ya tumbaku na pombe


      Matumizi ya vitu hivo vinaweza kupunguza uwezekano wa mwanamke kupata mimba.   Pia inaweza kusababisha mwanaume kusindwa kusababisha ujauzito kwa mwanamke.

5. Magonjwa ya mirija ya folopi na mji wa mimba.


     Magonjwa haya husababisha makovu katika mji wa mimba na na kufanya yai lililorutubishwa kutoweza kutungwa.

   Pia huweza kusababisha kuziba kwa mirija hiyo na kupelekea kuzuwia urutubishaji.
  Maranyingi magonjwa haya huwa ya zinaa ingawa kansa ya uzazi na ovari husababisha utasa pia.

6. Mwanaume wenye historia ya magonjwa kama tezi dume na maambukizi katika via vya uzazi pia yanaweza kupunguza uwezekano wa kusababisha mimba.
Add caption