Jumatano, 3 Mei 2017

Yajue magonjwa ya fangasi ya ngozi na matibabu yake

Magonjwa ya fangasi ya ngozi na matibabu yake

      Fangasi ni magonjwa yanayoathiri ngozi, kucha na nywele, pia huathiri mdomoni na ukeni. Magonjwa haya huambukiza kwa njia ya kugusana ua kshirikiana nguo hasa za ndani na tauro.

      Hapa tutaangalia fangasi katika kundi la magonjwa yanayoathiri ngozi, nywele na kucha (dermatomycosis).

      Kuna aina kuu 5 za magonjwa ya fangasi wa ngozi, nywele na kucha kama ifuatavyo;


  • Fangasi wa kichwani, ugonjwa huu huanza na sehemu ndogo ya ngozi ya kichwa na kukua kuwa sehemu kubwa. Huathiri nywele na kuzifanya dhaifu, laini na nyepesi kukatika au kung'oka. Huwaathiri sana watoti chini ya miaka 10 na hupotea mtu akisha barehe. Matibabu take  ni  griseofulvin na fluconazole, dozi zake huanzia siku 6-14.



  • Fangasi wa mwili, ugonjwa huu hutokea mwilini, sehemu ya ngozi iliyoathiriwa huwa nyekundu, duara kama shiringi na kukua huku ikiacha sehemu ya katikati kuwa na ngozi nzuri. Maduara haya yanaweza kukaa yakiwa kadhaa katika sehemu moja ya ngozi. Dawa nzuri kutumia ni za kupaka zinazokuwa katika tyubu, cotrimazole au ketoconazole. Kwa ugonjwa uliokua sana na kwa wagonjwa wenye kinga ya mwili ndogo kama wenye VVU, nivema wakatumia dawa ya kunywa




  • Fangasi wa nyayo na vidole, ugonjwa huu hutokea kama mabaka na kuchanika katikati ya vidole na huwacha sana na kuuma pia. Matibabu yake maranyingi huwa dawa ya kupaka kwa wiki 4, kwa ugonjwa uliokua sana tumia dawa ya kunywa kama griseofulvin kwa wiki 6-12.



  • Fangasi wa kucha, ugonjwa huu huathiri kucha na hubadilisha rangi ya kucha. Huzalishwa vitu kama chaki na ambavyo vikisuguliwa huweza kupukutika. Kucha huweza kulika na inaweza kuisha. Ili kutibu ugonjwa huu nibora kutumia dawa za kunjwa na terbinafine na itraconazole zimeonekana dawa bora zaidi.



  • Pityriasis, huu ni ugonjwa wa fangasi ambao huathiri sehemu ya huu sana ya ngozi katika sehemu za usoni, shingoni na mgongoni. Hutokea kama viduara vyenye mng'ao vinavyo washa. Huongezeka na huathiri sehemu kubwa ya ngozi visipotibiwa ingwa vinaweza kupotea vyenyewe. Maranyingi ugonjwa huu hauambukizwi Ila hutokea kama ajari tu yaapotikea mabadiliko fulani ya mwili. Sio ugonjwa hari sana kiafya ila haukubaliki kwani huharibu mwonekano wa mtu has a unapotokea maeneo ya uso na shingoni. Matibabu yake ni sawa na yale ya fangasi wa mwili.

Maoni 15 :

  1. Kuna fungus nyingine haziwashi Wala kuuma Ila zimetapakaa usoni shingon na mgongoni dawa yake nn???

    JibuFuta
  2. Mafunzo ni mazuri mngeweka na ushauri na tiba zake itakua vizuri

    JibuFuta
  3. Mwenye fangasi kati ya korodan na paja naye tatizo lake ni fangasi ya ngozi?

    JibuFuta
  4. Usinunue dawa, bila kupata vipimo na ushauli wa doctor!

    JibuFuta
  5. Mimi kuna tatizo moja huwa linajitokeza niki sex na wife nakuwa kama nachubuka then kesho yake napona na uume unaweka gamba jeusi sehem iliyo chubuka

    JibuFuta
    Majibu
    1. Nitafute kwa namba hizi 0744477776 kwa maelezo zadi na tiba

      Futa
  6. Nasubumbuliwa na fangasi tangu 2018 imenikumba maeneo ya mashavuni, inawasha, nimetumia dawa ya kumeza ila naona hali bado imejirudia.Je nifanyaje!

    JibuFuta
  7. asanten sana kwa matibabu

    JibuFuta
  8. Mimi ni mtu wa gym sana kuna fangasi mgongoni wa langi nyekundu dawa yake niniii?

    JibuFuta
  9. Free Spins on Live Casino Site
    The UK's number 1 online casino site offers great offers, amazing casino games and great promotions. 카지노사이트luckclub Read more about our promotions. Free Spins What are the most popular casino games?How do I claim free spins?

    JibuFuta