Jumamosi, 29 Aprili 2017

Jua ugonjwa wa kuoza fizi na namna ya kuuzuwia na kuutibu

Ugonjwa wa kuoza fizi

   Ugonjwa wa kuoza fizi ni ugonjwa unaotokea Mara chache na hutokea zaidi katika nchi zinazoendelea Kama Tanzania hasa katika maeneo ya watu maskini. Ugonjwa huwa hatari ikiwa utaendelea sana na kusababisha fizi kuozasana has a pale unapopelekea maambukizi ya magonjwa mengine.

Mambo yanayoweza kupelekea  ugonjwa huu

  • Kinywa kichafu, uchafu wa kinywa hupelekea kukua kwa bacteria hatari wanaoweza kupelekea ugonjwa.
  • Uvutaji sigara na matumizi ya ugoro na kubeli yanaweza kupelekea tatizo.
  • Afya mgogoro, mtu mwenye afya mgogoro anaweza kupelekea bacteria walio kinywani wasio na madhara kupelekea madhara na kusababisha ugonjwa.
  • Msongo wa mawazo
  • Kinga ya mwili kushuka kutokana sababu mbalimbali ukiwemo UKIMWI au magonjwa sugu kama kisukari.
  • Maambukizi ya magonjwa ya kinywa

Dalili za ugonjwa

Harufu mbaya ya kutoka kinywani na kuhisi radha mbaya
  • Damu kuvuja katika fizi kwa urahisi
  • Vidonda katika fizi
  • Kuvimba fizi na kuwa njekundu
  • Fizi kuuma
  • Fizi koza na kupukutika
  • Fizi kutokwa usaha

Matibabu 

Unapoona dalili za namna hii hapo juu, nivema uende hospitality ili ukaonane na daktari wa kinywa na meno, ikiwa unashindwa kuhospitali, fanya yafuatayo
  • Safisha kinywa chako kwa maji na kitambaa safi na laini
  • Nunua dawa ya kusukutua kinywani ( chlorhexidine ), sukutua kinywa chako kwa kufuata maelekezo utakayopewa unapoinunua.
  • Tumia amoxicycilne na paracetamol endapo unahisi msumivu ya fizi au homa, unaweza kiongeza metronidazole (frajiri) endapo tatizo ni kubwa. Tumia dozi ya Sikh tank kwa hili dawa isipokuwa paracetamol ambayo unaweza kutumia kwa Siku 3, hakikisha unafuata maelekezo ya matumizi ya dawa hizo uliyopewa wakati unazinunua.

Namna ya kukinga ugonjwa

Hakikisha unafanya usafi wa kinywa chako na kutembelea kliniki ya kinywa na meno walau Mara 2 kwa mwaka ili kupata ushauri, kukinga na kutibu magonjwa nyemerezi ya kinywa na meno.


Jumamosi, 22 Aprili 2017

Jua namna ya kumsaidia mtu aliepata mshituko

Ujue mshituko na namna ya kumsaidia mtu aliyepatwa na mshituko (Shock)


      Mshituko ni tatizo la kiafya linalompata mtu kutokana na kupungua kwa damu katika ubongo au kuathiliwa kwa mfumo wa fahamu. Tatizo hili linaweza kumpata mtu wa jinsia yoyote na umri wowote.

      Zipo aina tano za mshituko kama ifuatavyo;

  •   Mshituko unaosababishwa na  matatizo ya moyo
  • Mshituko unaoshababishwa na upungufu wa damu
  • Mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu 
  • Mshituko unaosababishwa na aleji
  • Mshituko unaosababishwa na kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu


   Mshituko unaosababishwa na moyo

       Moyo unaweza kushindwa kusukuma damu katika baadhi ya viungo kama ubongo na kupelekea kupungua kwa oksijeni katika ubongo, jambo hili linaweza kupelekea mshituko.
Moyo unaweza kushindwa kusukuma damu ipasavyo kutokana na magonjwa ya moyo.

Mshituko unaosababishwa na kupungua kwa damu

      Kupungua kwa damu katika mzunguko wake hupelekea kupungua
kwa kiwango cha damu inayosukumwa kuenda katika ubongo na kupelekea mshituko.
       Kupungua kwa damu katika mzunguko wake kunaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;

  • Kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi
  • Kuungua
  • Kuharisha
  • Maji kukimbilia sehemu za wazi za mwili kama zile zinazozunguka mapafu na tumbo

Mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu

      Hii hutokea pale bacteria wanapoingia katika damu na kumsikumo sumu. Sumu hii inapokua katika damu husababisha kulegea na kutanuka kwa mishipa ya damu. Mishipa ikitanuka hupunguza msukumo wa damu na kupelekea damu kushindwa kufika sehemu za juu za mwili hasa katika ubongo, jambo hili huweza kusababisha mshituko.

Mshituko unaosababishwa na aleji

      Hii hutokea pale chemikali toka nje ya mwili zinaposhindana na mwili na kusababisha kulegea na kutanuka kwa mishipa ya damu. Hali hii kupelekea kupungua msukumo wa damu na kufanya upungufu wa damu kufika katika ubongo na kupelekea mshituko.

Mshituko unaosababishwa na kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu

      Hii hutokea pale mtu anapopata msongo wa mawazo au uwoga, mfumo wa fahamu huweza kuathirika na kupelekea mshituko.

Dalili za mshituko


  • Ngozi baridi iliyopauka isipokuwa kwa mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu ambayo ngozi huwa yenye joto
  • Kuchanganyikiwa akili na kukosa utulivu
  • Kutokwa na jasho
  • Kutokupata mkojo
  • Kubadilika rangi na kuwa mweupe rangi inanyoonesha upungufu wa damu
  • Mgonjwa anaweza kupoteza fahamu
  • Pumzi ya chini na ya harakaharaka na mapigo ya moyo kuwa ya harakaharaka


Namna ya kumsaidia mgonjwa


  • Mweke mgonjwa katika sehemu yenye hewa safi na yakutosha
  • Regeza nguo za mwili wake
  • Mlaze mgonjwa chali na kichwa chake kikitazama upande kuruhusu mate kutokana nje ili asipakiwe, hii ni kwa mgonjwa alipoteza fahamu
  • Mlaze miguu yake ikiwa juu kidogo kichwa kikiwa chini kidogo kuruhusu damu kushuka katika ubongo
  • Akiwa katika hali nafuu apelekwe hospitali haraka ambako atapewa matibabu ikiwa ni pamoja na kuongezewa maji au damu na kupewa dawa.
  • Ikiwa mgonjwa amepata mshituko kwasababu ya kuvuja damu nyingi, inapasa kwanza kuzuwia damu kuvuja kisha huduma zingine zifuate ikiwa ni pamoja na kumuwahisha hospitali




Jumatatu, 3 Aprili 2017

Madhara ya utando mgumu katika meno

Jua madhara ya utando mgumu kwenye meno (calculus)


     Utando mgumu kwenye meno kwa jina la kitaalamu huitwa calculus,  utando huu huwa mgumu kiasi kwamba hauwezi kutoka kirahisi. Huwa na rangi tofauti tofauti kuanzia njano hadi nyeusi kutokana na hatua ya ukuaji wake.



     Calculus hutokea baada ya mabaki ya chakula yenye bacteria kwa wingi kukaa kwa muda ndefu hadi miezi kadhaa.

Madhara ya calculus 


1. Memo kuoza


     Utando huu huweka makazi mazuri kwa bacteria ambao hupelekea meno kuoza. Pia huweza kupelekea mabaki ya chakula kuongezeka na kuwawezesha hawa bacteria kujipatia chakula na makazi mazuri. Shughuli za bacteria hawa hupelekea jino kuoza katika eneo hilo.

      Kuoza meno kunaathari kubwa kiafya kwani kunaweza kupelekea kupoteza meno na magonjwa makubwa hata kupoteza maisha.

2. Fizi kushuka chini na kuacha mzizi wa jino wazi


   Calculus hupelekea fizi kushuka chini na kuacha mzizi wa jino wazi,  hii inaweza kupelekea kuhisi ganzi au maumivu ya jino kutokana na mzizi kuachwa wazi. Pia inaweza kupelekea jino kulegea na kufikia hata ya kung'olewa.


  3. Magonjwa ya fizi


     Calculus inaweza kupelekea magonjwa ya fizi kama gingivitis na periodontitis.   Gingivitis ni ugonjwa ambao hupelekea fizi kuvimba na kutokwa damu zinapo guswa kidogo.

     Periodontitis ni magonjwa ya fizi na mifupa ya taya, huambatana na fizi kuvuja damu, kuvimba,  kuoza na kutoa usaha. Pia hupeleke kulika kwa mfupa wa taya na kufanya meno kulegea.


4. Kusababisha magonjwa ya moyo


     Maambukizi ya bacteria huweza kupenya na kuingia katika mfumo wa mzunguko wa damu. Hii huweza kusababisha magonjwa ya moyo na dumu katika damu.
Namna ya kuzuwia calculus

     Ili kuzuwia utando huu,  hakikisha unapiga mswaki wako vizuri namna inayoruhusu pande zote za meno zinakuwa safi. Jifunze namna ya kupiga mswaki ili kuhakikisha usalama wa kinywa chako.


     Tembelea hospitali katika kliniki ya kinywa na meno ili utando huu uondolewe.   Ikiwa utando huu umeleta madhara katika afya yako, hakikisha utando huu unatolewa na matibabu yanatolewa ili kuzuwia ukuaji na madhara tatizo yanayoweza kujitokeza.
 

Kwamawasiliano piga; 
+255752674467
+255676674467