Jua madhara ya utando mgumu kwenye meno (calculus)
Utando mgumu kwenye meno kwa jina la kitaalamu huitwa calculus, utando huu huwa mgumu kiasi kwamba hauwezi kutoka kirahisi. Huwa na rangi tofauti tofauti kuanzia njano hadi nyeusi kutokana na hatua ya ukuaji wake.
Calculus hutokea baada ya mabaki ya chakula yenye bacteria kwa wingi kukaa kwa muda ndefu hadi miezi kadhaa.
Madhara ya calculus
1. Memo kuoza
Utando huu huweka makazi mazuri kwa bacteria ambao hupelekea meno kuoza. Pia huweza kupelekea mabaki ya chakula kuongezeka na kuwawezesha hawa bacteria kujipatia chakula na makazi mazuri. Shughuli za bacteria hawa hupelekea jino kuoza katika eneo hilo.
Kuoza meno kunaathari kubwa kiafya kwani kunaweza kupelekea kupoteza meno na magonjwa makubwa hata kupoteza maisha.
2. Fizi kushuka chini na kuacha mzizi wa jino wazi
Calculus hupelekea fizi kushuka chini na kuacha mzizi wa jino wazi, hii inaweza kupelekea kuhisi ganzi au maumivu ya jino kutokana na mzizi kuachwa wazi. Pia inaweza kupelekea jino kulegea na kufikia hata ya kung'olewa.
3. Magonjwa ya fizi
Calculus inaweza kupelekea magonjwa ya fizi kama gingivitis na periodontitis. Gingivitis ni ugonjwa ambao hupelekea fizi kuvimba na kutokwa damu zinapo guswa kidogo.
Periodontitis ni magonjwa ya fizi na mifupa ya taya, huambatana na fizi kuvuja damu, kuvimba, kuoza na kutoa usaha. Pia hupeleke kulika kwa mfupa wa taya na kufanya meno kulegea.
4. Kusababisha magonjwa ya moyo
Maambukizi ya bacteria huweza kupenya na kuingia katika mfumo wa mzunguko wa damu. Hii huweza kusababisha magonjwa ya moyo na dumu katika damu.
Namna ya kuzuwia calculus
Ili kuzuwia utando huu, hakikisha unapiga mswaki wako vizuri namna inayoruhusu pande zote za meno zinakuwa safi. Jifunze namna ya kupiga mswaki ili kuhakikisha usalama wa kinywa chako.
Tembelea hospitali katika kliniki ya kinywa na meno ili utando huu uondolewe. Ikiwa utando huu umeleta madhara katika afya yako, hakikisha utando huu unatolewa na matibabu yanatolewa ili kuzuwia ukuaji na madhara tatizo yanayoweza kujitokeza.
Kwamawasiliano piga;
+255752674467
+255676674467
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni