Jumamosi, 22 Aprili 2017

Jua namna ya kumsaidia mtu aliepata mshituko

Ujue mshituko na namna ya kumsaidia mtu aliyepatwa na mshituko (Shock)


      Mshituko ni tatizo la kiafya linalompata mtu kutokana na kupungua kwa damu katika ubongo au kuathiliwa kwa mfumo wa fahamu. Tatizo hili linaweza kumpata mtu wa jinsia yoyote na umri wowote.

      Zipo aina tano za mshituko kama ifuatavyo;

  •   Mshituko unaosababishwa na  matatizo ya moyo
  • Mshituko unaoshababishwa na upungufu wa damu
  • Mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu 
  • Mshituko unaosababishwa na aleji
  • Mshituko unaosababishwa na kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu


   Mshituko unaosababishwa na moyo

       Moyo unaweza kushindwa kusukuma damu katika baadhi ya viungo kama ubongo na kupelekea kupungua kwa oksijeni katika ubongo, jambo hili linaweza kupelekea mshituko.
Moyo unaweza kushindwa kusukuma damu ipasavyo kutokana na magonjwa ya moyo.

Mshituko unaosababishwa na kupungua kwa damu

      Kupungua kwa damu katika mzunguko wake hupelekea kupungua
kwa kiwango cha damu inayosukumwa kuenda katika ubongo na kupelekea mshituko.
       Kupungua kwa damu katika mzunguko wake kunaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;

  • Kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi
  • Kuungua
  • Kuharisha
  • Maji kukimbilia sehemu za wazi za mwili kama zile zinazozunguka mapafu na tumbo

Mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu

      Hii hutokea pale bacteria wanapoingia katika damu na kumsikumo sumu. Sumu hii inapokua katika damu husababisha kulegea na kutanuka kwa mishipa ya damu. Mishipa ikitanuka hupunguza msukumo wa damu na kupelekea damu kushindwa kufika sehemu za juu za mwili hasa katika ubongo, jambo hili huweza kusababisha mshituko.

Mshituko unaosababishwa na aleji

      Hii hutokea pale chemikali toka nje ya mwili zinaposhindana na mwili na kusababisha kulegea na kutanuka kwa mishipa ya damu. Hali hii kupelekea kupungua msukumo wa damu na kufanya upungufu wa damu kufika katika ubongo na kupelekea mshituko.

Mshituko unaosababishwa na kuathiriwa kwa mfumo wa fahamu

      Hii hutokea pale mtu anapopata msongo wa mawazo au uwoga, mfumo wa fahamu huweza kuathirika na kupelekea mshituko.

Dalili za mshituko


  • Ngozi baridi iliyopauka isipokuwa kwa mshituko unaosababishwa na maambukizi ya damu ambayo ngozi huwa yenye joto
  • Kuchanganyikiwa akili na kukosa utulivu
  • Kutokwa na jasho
  • Kutokupata mkojo
  • Kubadilika rangi na kuwa mweupe rangi inanyoonesha upungufu wa damu
  • Mgonjwa anaweza kupoteza fahamu
  • Pumzi ya chini na ya harakaharaka na mapigo ya moyo kuwa ya harakaharaka


Namna ya kumsaidia mgonjwa


  • Mweke mgonjwa katika sehemu yenye hewa safi na yakutosha
  • Regeza nguo za mwili wake
  • Mlaze mgonjwa chali na kichwa chake kikitazama upande kuruhusu mate kutokana nje ili asipakiwe, hii ni kwa mgonjwa alipoteza fahamu
  • Mlaze miguu yake ikiwa juu kidogo kichwa kikiwa chini kidogo kuruhusu damu kushuka katika ubongo
  • Akiwa katika hali nafuu apelekwe hospitali haraka ambako atapewa matibabu ikiwa ni pamoja na kuongezewa maji au damu na kupewa dawa.
  • Ikiwa mgonjwa amepata mshituko kwasababu ya kuvuja damu nyingi, inapasa kwanza kuzuwia damu kuvuja kisha huduma zingine zifuate ikiwa ni pamoja na kumuwahisha hospitali




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni