Ijumaa, 10 Februari 2017

kutokwa harufu mbaya mdomoni

Je, unazijua sababu za kutokwa harufu mbaya mdomoni?




   Tatizo hili linawakabili watu wengi, katika jamii ya kitanzania, kati ya watu wanne basi mmoja anaweza kuwa anakabiliana na tatizo hili japo kwa kiwango tofauti.
 
   Wapo wanaojigundua kuwa wanatatizo na wengine hawajigundui mpaka atapoambiwa na jirani yake ama mpenzi wake. Maranyingi watu hushindwa kuwaambia wenzao endapo wamegundua kuwa mwenzao anatatizo hilo kwani ni la aibu hivo kushindwa kujitambua.

   Wengine hawagunduliki kutokana na tatizo kuwa dogo kwao yani harufu kuwa kidogo sana mpaka pale tu anaposogelewa zaidi na mwenzake.

   Urafiki au mapenzi ya watu yanaweza kuvunjiki ikiwa mmojawapo akiwa na tatizo hilo, hivo fuatana nami ujue kwanini tatizo hilo linatokea, namna ya kuzuwia na kutibu.

Sababu zinazoweza kupelekea tatizo hili
    Zipo sababu kadhaa zinazo weza kusababisha tatizo la kutoa harufu mdomoni, hapa tutaangalia chache tu ambazo zinaweza kukusaidia kwa sehem kubwa.

1. Kuto kuweka kinywa (mdomo) katika hali ya usafi.
   Kinywa kisipo safishwa hubaki na mabaki ya chakula ambayo huvunjwavunjwa na bacteria na kuzalisha kemikali zinazo sababisha harufu mbaya. Bacteria huweza kuvunjavunja mabaki kwa kasi kutegemaeana na wingi wake na hali ya kinywa.

   Njia kuu za kuweka kinywa safi ni pamoja na kupiga mswaki na kuchokonoa meno kwa vijiti (sticks).

   Baadhi ya watu hawajui kupiga mswaki kwani hushindwa kufikia baadhi ya kuta za meno hasa magego ya mwisho hivo tatizo la harufu mbaya kuendelea.

   Kitaalam inashauliwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku, asubuhi kabla au baada ya chai na baada ya chakula cha jioni yaani kabla ya kulala. Ili kulinda meno zaidi nivema kutosukutua kwa maji baada ya kupiga mswaki.

2. Uvutaji wa sigara namatumizi ya mazao ya tumbaku kama vile kubeli na ugoro vinaweza kuwa sababu ya kutoka harufu kinywani.

3. Matumizi ya baadhi ya vyakula vinavyotoa harufu mbaya kama vitunguu swaumu na matumizi ya pombe. Nivema kupiga mswaki au kutafuna chakula chenye harufu nzuri kama bigijii na pipi baada ya kutumia vyakula kama vitunguu swaumu.

4. Magonjwa ya fizi na taya (periodontitis).
    Yapo magonjwa yanayoweza kusababisha kutoa harufu hasa kwa mtu mwenye ugonjwa wa kuozesha fizi (necrotizing gingivitis) au majipu ya fizi. Kutokana na shughuli za bacteria katika hizi fizi, harufu huzalishwa.

5. Magonjwa ya njia za hewa na mapafu pia huweza kusababisha harufu mbaya kutoka kinywani.

Namna ya kukinga
   Namna ya kukinga tatizo hili inategemeana na sababu iliyopelekea tatizo hili. Hizi hapa ni njia za kuzuwia na kuondoa tatizo hili:

   Kuhakikisha kinjwa kinakuwa safi kwa kupiga mswaki kila pande za kila jino na kupitisha mswaki juu ya ulimi. Unaweza kutumia wastani wa dakika 5 kuhakikisha umepiga mswaki vizuri.

   Tumia vijiti kuchokonoa meno ili kuondoa mabaki kati ya meno ambapo mswaki hauwezi kupita. Hilo linatakiwa kufanyika taratibu kuzuwia kujiumiza fizi.

   Kusukutua kwa aina ya dawa ya maji (antibacterial mouth rinse), hii inaweza kupatikana katika maduka ya madawa au hospitali na katika vituo vya afya.

   Tumia vyakula vyenye harufu nzuri baada ya kutumia vile vyenye harufu mbaya.

   Acha matumizi ya sigara na mazao yake kama kubeli.

   Nenda hospitaliti na umwone daktari wa kinywa na meno endapo unahisi kuwa harufu ya kinywa chako inatokana na magonjwa ya fizi au mingineyo.



Ili kufaham zaidi kuhusu afya ya kinywa na meno, endelea kufuatana nami katika makala mbali mbali au piga  simu:
+255752674467 au
+255676674467
JINA: Ibrahim Mamboleo

Maada zinazo fanana
>Afya ya mama ma mtoto
>Afa ya uzazi na mahusiano
Afya ya mwili na akili nk

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni