Jumatatu, 27 Februari 2017

Ongeza uwezo wa ubongo wako kwa kufanya haya

Jifunze namna ya kuongeza uwezo wa akili yako


     Watu wingi huamini kuwa uwezo wa ubongo hupungua mtu anavo kuwa, lakini ubongo wa binadam huweza kuendelea na kazi yake vizuri tu hadi uzeeni endapo ubongo utakuwa na hali nzuri kiafya. Kwani seli za ubongo huweza kuzalishwa ikiwa utakuwa na afya njema.

     Ili kuongeza uwezo wa ubongo wako yapo mambo muhimu ya kuzingatia. Mambo haya yatasaidia ubongo wako kuwa imara kwani uwezo wa kufanya kazi kama uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu utaongezeka.

     Yafuatayo yatasaisia ubongo wako kufanya kazi kwa ufanisi zaidi hadi katika hali ya uzee.


1. Kucheka na kufurahi


      Moja kati ya vitu muhimu ili kufanya afya ya akili kuwa safi ni kupata nafasi ya kucheka na kufurahi. Kucheka hufanya kuzalishwa kwa seli za akili ambazo hufanya ubongo kuendelea kudumu kuwa na ngufu hadi uzeeni.

     Nivema kutafuta fulsa mbalimbali zitakazo kiwezesha kucheka na kufurahi katika mazingira mbalimbali ya maisha yako.

2. Kuvuta pumzi ndefu


     Kuvuta pumzi ndefu husaidia kupandisha dumu juu ikiwemo katika ubongo, pia husaidia kupunguza uwoga pale unapotarajia kufanya jambo.

     Nivema kwa siku baadhi kuwa unapata nafasi ya kuenda sehemu tulivu pekeyako na kukaa kisha unavuta pumzi ndefu na kushusha. Zoezi hili unaweza kulifanya ndani ya dakika 5 dadi 10.

     Baada ya hapo unaweza kuendelea kutulia na unaweza kufumba macho ukisikia sauti za ndege, au maji yanayo tembea au sauti za magari huku ukitafakari.

     Pia unaweza kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuanza mtihani wako ili kupandisha damu juu na kupunguza woga wa mtihani.

3. Kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii


     Inatakiwa mtu asiwe wa kukaa pekeyake bila kushiriki mambo ya kijamii kama yakidini, misiba au kubdilishana mawazo mbalimbali.

     Kushiriki mambo ya kijamii huimarisha akili na kufanya kuwa yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi pale inapo hitajika. Hii huambatana na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo za pamoja.

4. Kuchangamsha na kuburudisha akili akili


      Kunawakati akili huhitajika kuburudishwa na kuchangamshwa kwa kufanya mambo kama vile kutalii mbuga za wanyama, kutoka na familia kujivinjari, kuangalia michezo ya video, kucheza wimbo au kucheza gemu.

     Kuchangamsha akili huifanya akili yako iweze kujijenga vizuri zaidi.

5. Kuipatia akili changamoto


      Ili kuongea uzalishaji wa seli za ubongo na kuifanya akili yako kuwa imara na uwezo wa kutunza kumbukumbu, akili inahitajika kupewa changamoto na sio kuishi bila kufanya akili kuweza kujishughilisha. Changamoto hizo ni kama kujifunza kitu kipya kama lugha, kupiga kinanda au gitaa au kupata habari mbalimbali za ulimwengu.

6. Kulala


     Kulala ni muhimu kwani hupumzisha akili yako, ikiwa umelala na mambo kichwani huyapanga vizuri ili kufa yawekwe katika kumbukumbu nzuri. Pia huweza kuuandaa ubongo vizuri kwaajiri ya kupokea mambo mapya.

      Nivizuri kwa mtu mzima kulala kati ya masaa 7.5 ha 8.5, na nivizuri zaidi ikawa utalala usingizi wa usiku usio na ghasia za kushituliwa kutoka usingizini.

7. Kurudiarudia jambo na kulihusianiasha na uhalisia


     Kurudiarudia jambo huweza kufanya kumbukumbu yake isipotee kwa wepesi. Na nivema zaidi jambo jipya kurudiwa tena siku hiyohiyo ili kuliingiza katika kumbukumbu ya muda mrefu.

     Pia jambo geni linaweza kuhusianishwa na linalofahamika ili kufanya jambo jipya kudumu akilini. Mfano unaweza kuandika kifupi cha maneno ya kile unachojifunza, nakifupi hicho kinakuwa na maana fulani inayo fahamika.


8. Mazoezi ya viungo


     Mazoezi ya viungo husaidia akili kuwa imara kwa husaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa seli za ubongo. Pia mazoezi huasaidia kupandisha damu kwenye ubongo na kuufanya kupata chakula na oksijeni ya kutosha. Ubongo hutumia 20% ya oksijeni yote ya mwilini hivyo ongezeko lake kuongeza ufanisi wa ubongo.

     Mazoezi husaidia kupunguza uwezekano wa magonjwa ya mishipa ya damu na moyo na kisukari, kutokana na magonjwa hayo kuhafifisha ufanisi wa utendaji wa ubongo, kuyazuwia huweza kuongeza nguvu ya ubongo na akili.


9. Kupata chakula kinachoimarisha ubongo


   Chakula chenye wingi wa omega-3-fati kama vile samaki, ini, ubongo na vinginevyo husaidia kimarisha ubongo. Kutokana na mwili kutokuwa na uwezo wa kuzalisha vyakula hivo, inahitajika kula kutoka kwa vyanzo vingine kama samaki.

   Ili kuboresha ufanisi wa kazi ya ubongo na akili, fanya mambo hayo kama yanavo jieleza.

Endelea kufuatana nami katika mambo mbalimbali ya afya kupitia blog yangu au piga simu;
0752674467
0676674467
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni