Jumamosi, 4 Machi 2017
Jumatatu, 27 Februari 2017
Ongeza uwezo wa ubongo wako kwa kufanya haya
Jifunze namna ya kuongeza uwezo wa akili yako
Watu wingi huamini kuwa uwezo wa ubongo hupungua mtu anavo kuwa, lakini ubongo wa binadam huweza kuendelea na kazi yake vizuri tu hadi uzeeni endapo ubongo utakuwa na hali nzuri kiafya. Kwani seli za ubongo huweza kuzalishwa ikiwa utakuwa na afya njema.
Ili kuongeza uwezo wa ubongo wako yapo mambo muhimu ya kuzingatia. Mambo haya yatasaidia ubongo wako kuwa imara kwani uwezo wa kufanya kazi kama uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu utaongezeka.
Yafuatayo yatasaisia ubongo wako kufanya kazi kwa ufanisi zaidi hadi katika hali ya uzee.
1. Kucheka na kufurahi
Moja kati ya vitu muhimu ili kufanya afya ya akili kuwa safi ni kupata nafasi ya kucheka na kufurahi. Kucheka hufanya kuzalishwa kwa seli za akili ambazo hufanya ubongo kuendelea kudumu kuwa na ngufu hadi uzeeni.
Nivema kutafuta fulsa mbalimbali zitakazo kiwezesha kucheka na kufurahi katika mazingira mbalimbali ya maisha yako.
2. Kuvuta pumzi ndefu
Kuvuta pumzi ndefu husaidia kupandisha dumu juu ikiwemo katika ubongo, pia husaidia kupunguza uwoga pale unapotarajia kufanya jambo.
Nivema kwa siku baadhi kuwa unapata nafasi ya kuenda sehemu tulivu pekeyako na kukaa kisha unavuta pumzi ndefu na kushusha. Zoezi hili unaweza kulifanya ndani ya dakika 5 dadi 10.
Baada ya hapo unaweza kuendelea kutulia na unaweza kufumba macho ukisikia sauti za ndege, au maji yanayo tembea au sauti za magari huku ukitafakari.
Pia unaweza kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuanza mtihani wako ili kupandisha damu juu na kupunguza woga wa mtihani.
3. Kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii
Inatakiwa mtu asiwe wa kukaa pekeyake bila kushiriki mambo ya kijamii kama yakidini, misiba au kubdilishana mawazo mbalimbali.
Kushiriki mambo ya kijamii huimarisha akili na kufanya kuwa yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi pale inapo hitajika. Hii huambatana na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo za pamoja.
4. Kuchangamsha na kuburudisha akili akili
Kunawakati akili huhitajika kuburudishwa na kuchangamshwa kwa kufanya mambo kama vile kutalii mbuga za wanyama, kutoka na familia kujivinjari, kuangalia michezo ya video, kucheza wimbo au kucheza gemu.
Kuchangamsha akili huifanya akili yako iweze kujijenga vizuri zaidi.
5. Kuipatia akili changamoto
Ili kuongea uzalishaji wa seli za ubongo na kuifanya akili yako kuwa imara na uwezo wa kutunza kumbukumbu, akili inahitajika kupewa changamoto na sio kuishi bila kufanya akili kuweza kujishughilisha. Changamoto hizo ni kama kujifunza kitu kipya kama lugha, kupiga kinanda au gitaa au kupata habari mbalimbali za ulimwengu.
6. Kulala
Kulala ni muhimu kwani hupumzisha akili yako, ikiwa umelala na mambo kichwani huyapanga vizuri ili kufa yawekwe katika kumbukumbu nzuri. Pia huweza kuuandaa ubongo vizuri kwaajiri ya kupokea mambo mapya.
Nivizuri kwa mtu mzima kulala kati ya masaa 7.5 ha 8.5, na nivizuri zaidi ikawa utalala usingizi wa usiku usio na ghasia za kushituliwa kutoka usingizini.
7. Kurudiarudia jambo na kulihusianiasha na uhalisia
Kurudiarudia jambo huweza kufanya kumbukumbu yake isipotee kwa wepesi. Na nivema zaidi jambo jipya kurudiwa tena siku hiyohiyo ili kuliingiza katika kumbukumbu ya muda mrefu.
Pia jambo geni linaweza kuhusianishwa na linalofahamika ili kufanya jambo jipya kudumu akilini. Mfano unaweza kuandika kifupi cha maneno ya kile unachojifunza, nakifupi hicho kinakuwa na maana fulani inayo fahamika.
8. Mazoezi ya viungo
Mazoezi ya viungo husaidia akili kuwa imara kwa husaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa seli za ubongo. Pia mazoezi huasaidia kupandisha damu kwenye ubongo na kuufanya kupata chakula na oksijeni ya kutosha. Ubongo hutumia 20% ya oksijeni yote ya mwilini hivyo ongezeko lake kuongeza ufanisi wa ubongo.
Mazoezi husaidia kupunguza uwezekano wa magonjwa ya mishipa ya damu na moyo na kisukari, kutokana na magonjwa hayo kuhafifisha ufanisi wa utendaji wa ubongo, kuyazuwia huweza kuongeza nguvu ya ubongo na akili.
9. Kupata chakula kinachoimarisha ubongo
Chakula chenye wingi wa omega-3-fati kama vile samaki, ini, ubongo na vinginevyo husaidia kimarisha ubongo. Kutokana na mwili kutokuwa na uwezo wa kuzalisha vyakula hivo, inahitajika kula kutoka kwa vyanzo vingine kama samaki.
Ili kuboresha ufanisi wa kazi ya ubongo na akili, fanya mambo hayo kama yanavo jieleza.
Endelea kufuatana nami katika mambo mbalimbali ya afya kupitia blog yangu au piga simu;
0752674467
0676674467
Jumanne, 21 Februari 2017
Namna ya kumpata mtoto wa kiume au wa kike
Jua namna ya kumpata mtoto wa kiume au wa kike
Watu wingi wamekuwa wakitamani kupata mtoto wa jinsia fulani kutokana na kupata watoto wa jinsia moja tu. Wengine hutamani mara tu baada ya kuingia katika ndoa wapate mtoto wa jinsia wanayoipenda.
Iko wazi kuwa kuzaa mtoto wa jinsia fulani ni mpango wa mwenyezi Mungu, lakini mwanadamu amepewa sehemu kidogo sana ya kukamilisha uumbaji. Kwasababu hiyo kukawa na wanasayansi ambao hufunuliwa vitu vichache ili kila mwenye kutaka kujifunza aweze kukamilisha uumbaji wake. Hivo wewe pia unanafasi ya kufanya kitu kwa sehemu fulani kikawa na hujachela.
Iko wazi kuwa mtu anaweza kupanga na mwenzi wake wazae mtoto wa jinsia gani kwa wakati gani. Kwakuwa sisi wanadamu sio waumbaji, hili huwa ni kwa uwezekano (probability) na ukiwa makini kabisa kunakuwa na uwezekano mkubwa sana wa kupata kile ulicho hitaji kuliko vinginevyo.
Ili kujua namna ya kupata mtoto wa jinsia fulani, unatakiwa kwanza kujua niwakati gani unaweza kupata mtoto.
Soma kwa makini mchoro hapo chini kisha ufuatane nami katika maelezo yanayo fuata.
Wakati wa kushika ujauzito
Mzunguko wa hedhi ya mwanamke iliyo sawia hukamilika kwa siku 28. Kwa kawaida wanawake wengi huwa na hedhi yenye mzunguko wa siku 28 hadi 32, ingawa wapo wengine huwa na mzunguko mfupi wa siku 14 hadi 25 na wengine mrefu zaidi hadi kufikia siku 42.
Hapa tutaongelea mtu mwenye mzunguko wa siku 28.
Siku ya kwanza huanza kuhesabiwa pale tu mwanamke anapoingia hedhi, kama ameingia tarehe 8 basi tarehe hiyo itakuwa siku ya kwanza ya mzunguko wake, na mzunguko wake utaisha pale atapoingia hedhi inayofuata.
Mfano, akiingia tarehe 8 mwezi wa tano na kuingia tena tarehe 6 mwezi wa sita, basi mzunguko wake utakuwa una siku 29. Kumbuka siku ya kwanza kuingia hedhi ya mwezi unaofuata haihesabiwi katika mzunguko ulionao kwa wakati huo, huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko unaofuata.
Mwanamke anaweza kuingia hedhi na siku ya tano akatoka, siku ya Kumi na moja ndipo uwezekano wa kushika mimba huanza kuwa. Hii ni kutokana na kukomaa kwa yai lake na kuwa pevu na hutalajia kutoka katika ovari.
Wastani wa siku anayoingia katika mwezi mpevu (ovulation) ni siku ya 14. Yai hili huweza kukaa masaa 12 hadi 24, baada ya hapo hufunga na kuto kuruhusu urutubishaji.
Mbegu za mwanaume huweza kukaa hadi siku tatu tangu kuingia katika via vya uzazi vya mwanamke, baada ya hapo huharibika. Kutokana na hilo mwanamke anae tarajia kuingia mwezi mpevu siku ya 13 au 14 akikutana na mwanaume siku ya 11 au 12 anaweza kushika mimba.
Mwanamke aliyeingia mwezi mpevu siku ya 14 au 15 akikutana na mwanaume siku ya 15 au 16 anaweza kushika mimba.
Mwanamke akikutana na mwanaume siku ya 14 huwa na uwezekano mkubwa sana wa kushika mimba. Uwezekano wa kushika mimba huongezeka kutoka siku ya 11 hadi 14, na huanza kupungua tena kutoka siku hiyo hadi ya 16.
Uwezekano wa kushika mimba siku ya 1 hadi ya 10 huwa mdogo mno, kuanzia siku ya 17 hadi 28 pia uwezekano huwa mdogo mno. Mimba inapotokea katika vipindi hivo huwa kuna sababu nyingine zinazo pelekea.
Namna ya kumpata mtoto wa kike
Anza rasmi kukutana na mpenzi wako siku ya 11 na 12. Katika siku ya 11 anza kuweka mbegu hata mara moja tu au mara mbili, ui pizi maranyingi sana acha nafasi ukutane nae siku ya 12.
Baada ya hapo mwache ili akiingia mwezi mpevu, yai lake likutane na mbegu zilizo himili kuendelea kuwepo ambazo huwa x, hizo huishi muda mrufu na kuvumilia hali na ndizo husababisha mtoto wa kike.
Namna ya kumpata mtoto wa kiume
Nivema kukutana usiku wa kuamkia siku ya 14 na siku ya 14 yenyewe. Pia ukikutana nae siku ya 15 au 16 ikawa yai lake bado halijafunga, unaweza kupata mtoto wa kiume.
Hii ni kutokana na mbegu za kiume kuwa na wepesi wa kuenda na kukutana na yai lililo tayari pevu. Yai linapokuwa tayari mbegu y huwa na uwezekano mkubwa sana wa kurutubisha yai hilo na kusabisha mtoto wa kiume.
Kutokana na mbegu hizi kutokuwa na ustahimilivu wa hali, hakikisha unakutana na mwanamke ambaye yuko vizuri kisaikolijia, anaefurahia tendo la ndoa. Upatikane muda mrefu wa kumuandaa ili azalishe ute mwingi utakao saidia mbegu kusafiri kwa wepesi na usalama mpaka katika mirija ya folopia ambako urututushaji hufanyikia.
Sio mbegu zote zinazoweza kufika katika eneo la urutubishaji nyingi hufia nyiani, ni chache na nyingi huwa za kikehasa pale mazingira yapokuwa si mazuri. Za kiume huwa hodari zaidi mazingira yanapo kuwa mazuri ingawa maisha yake huwa mafupi.
NB: Uwezekano wa kupata mtoto wa kiume au wa kike huwa kwa mwanaume, yeye ndo anaweza sababisha mabadiliko yoyote ingawa mwanamke mwenye ushirikiano mzuri kwa mwanaume humwongezea mwanaume uwezekano wa kumpata mtoto anaemtaka.
Endelea kufuatana nami, au piga simu
0752674467
0676674467
ibrahimmamboleo09@gmail.com
Jumapili, 19 Februari 2017
sababu zinazo pelekea kushindwa kushika ujauzito
Sababu zinazo weza kuzuwia mimba kutunga
Watu wengi hudhani kuwa niwakati tu umri umeenda ndo sababu ya mwanamke kushindwa kushika mimba. Nawengine hulaumu wanawake kwanini hawazai bila kujua sababu zinazo weza pelekea hali hiyo.
Zipo sababu zinazoweza kupelekea mwanamke asishike mimba, nyingine zikiwa zinachangiwa na mwanaume na nyingine mwanamke mwenyewe.
Sababu zinazoweza kupelekea hali hii
1. Mtindo wa maishaIpo mitindo ya maisha ambayo hushusha afya ya mtu kama vile uvutaji sigara, matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye caffeine kwa wingi, bangi, ulevi na utumiaji wa madawa mengine ya kulevya.
Hii hupelekea kupunguza uwezekano wa kutunga mimba na inamuathiri mtu wa jinsia yoyote.
Maisha haya yanaweza kupelekea uzalishaji wa mbegu zisizo komaa au mbegu kidogo za kiume na kupunguza uwezekano wa urutubishaji.
2. Magonjwa ya zinaa
Magonjwa ya zinaa yaliyomengi huwa hayaoneshi dalili kwa wanawake hivo yanapo kuwa hayajatibiwa huweka makovu katika mji wa mimba.
Hili hupelekea mimba kutotungwa hatakama urutubishaji wa yai la mwanamke umeshafanyika.
Pia magonjwa ya zina yanaweza kuathiri mirija ya mwanaume ya kupitisha mbegu ikapelekea asitoe mbengu wakati wa tendo la ndoa.
3. Magonjwa ya mji wa mimba na mirija ya folopia
Majonjwa yanayo athiri mirija ya folopia kama Kansa na baadhi ya magonjwa ya zinaa, yanaweza kupelekea kuziba kwa mirija hiyo. Hili huzuwia mbegu za kiume kukutana na yai ili kurutubisha.
Pia magonjwa haya huweza kusababisha makovu na kuongezeka kwa ukuta wa mji wa mimba, kutokana na hili mimba inashindwa kutungwa.
Wakati mwingine Kansa inaweza kuathiri ovari ambazo ndizo huhusika na uzalishaji wa mayai ya kike.
4. Homoni kushindwa kuwa na uwiano sawa
Kutokuwa na mpangilio unaoeleweka wa majira ya mzunguko wa hedhi kwa mwanamke hutokana na kutokuwa na mpangilio sahihi wa homoni. Hii inaweza kufanya wakati halisi wa kushika mimba usijulikane na kupelekea mimba kutotungwa kwa wakati wapenzi wanapo hitaji mtoto.
5. Unene
Mwanamke akiwa na uzito na unene mkubwa anaweza sababisha kutotungwa kwa mimba kutokana uwezekano wa kuzalisha kiwango kikubwa cha homoni oestrojeni inayozuwia mimba kutungwa.
6. Umri
Mwanamke anapofikia umri wa miaka 43, uwezekano wa yeye kushika mimba huwa mdogo. Kwakadri umri wa mwanamke unavyoongezeka na idadi na ubora wa mayai yake hupungua pia.
7. Chakula
Mwanamke anaekosa afya nzuri kutokana na upungufu wa virutubisho mwilini hupunguza uwezekano wa kushika mimba.
8. Madawa
Badhi ya madawa kama yanayotumika kipunguza maumivu na kutibu magonjwa sugu kama kansa yanaweza kusababisha kupungua kwa uwezekano wa mwanamke kushika mimba.
9. Kutoelewa wakati wa kushika mimba
Baadhi ya watu hushindwa kujua wakati sahihi wa mwanamke kushika mimba. Hii hupelekea wapenzi kukutana wakati ambao sio muafaka na kufanya wakakaa muda mrefu bila kupata mtoto.
Wapenzi wanaweza kishi kwa miaka kadhaa kisha wakapata mtoto au wanaweza kuza mwanzo kisha hali ya kutoshika mimba ikajitokeza, moja kati ya sababu hizo inaweza sababiash na sio ajabu.
Inahita kukaa chini mwanake na mwanaume kuona tatizo linaweza kuwa nini, na sio kumwachia mwanmake pekeyake.
Endelea kufuatana nami katika maada mbalimbali au piga simu:
0752674467
0676674467
Vyakula kwaajiri ya afya ya ngozi
Jua vyakula 10 kwa afya ya ngozi yako
Afya ya ngozi ni jambo ambalo kilamtu anahitajika uitunza na kuiimarisha ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya ngozi na kuongeza mvuto wa ngozi yake kwa watu. Watu wengi wamekuwa wakitafuta vipodozi mbalimbali ili kujichubua ngozi zao jambo ambalo huhatarisha afya ya ngozi zao na kupelekea magonjwa mbali mbali ya ngozi ikiwamo kansa ya ngozi.
Fuatana nami ili kujua namna ya kuifanya ngozi yako kuwa yenye afya, mvuto na rangi yake asili.
Vipo vyakula Vingi ambavyo vikitumiwa vizuri hufanya ngozi yako kuwa bora zaidi, hapa tutajadili vyakula Kumi muhimu ili kuimarisha ngozi yako.
1. Viazi vitamu
Viazi vitamu vina wingi wa vitamini A ambayo hupunguza ngozi kukunjamana na kuondoa dalili za uzee.
2. Parachichi
Tunda hili lina wingi wa viamini A na C na nyuzinyuzi, virutubisho hivi husaidia kuzuwia mikunjamano ya ngozi, ngozi kuzeeka mapema, kukinga dhidi ya maradhi na nyuzinyuzi husaidia mmeng'enyo wa virutubisho hivo.
3. Vyakula vya ngano
Vyakula vya ngano kama mkate, chapati au ngano iliyo chemshwa hulinda, kuimarisha ngozi nakuifanya kuwa laini. Inashauliwa kutumia vyakula vya ngano ya kahawia na sio nyeupe ili kuimalisha mmeng'enyo wa chakula na afya yako.
4. Samaki
Katika samaki kuna wingi wa protini na vitamini B12 muhimu kumarisha ngozi yako na kuifanya laini na yenye mvuto.
5. Chungwa
Chungwa ni tunda muhimu kwa ngozi yako kwani huilinda ngozi dhidi ya mionzi ya jua ambayo huathiri ngozi. Utafiti uliofanyika na chuo cha Arizona ulionesha kuwa 33% ya watu waliotumia sana machungwa walijilinda dhidi ya mionzi ya jua inayoathiri ngozi.
6. Karoti
Karoti huimarisha ngozi na kifanya iwe na mvuto zaidi kutokana na kuwa na wingi wa carotenoid ambayo huimarisha ngozi na kuifanya iwe na afya nzuri na ranging inayovutia.
7. Chokoleti (chocolate)
Chokoleti huisaidia ngozi kuwa yenye unyevu na laini, hii huifanya ngozi iwe kama imepakwa kipodozi kwani huwa na mng'o wenye mvuto.
8. Boga
Maboga huwa na wingi wa beta-carotine ambayo hubadilishwa na kuwa vitamini A ambayo hufanya ngozi yako kuwa yenye afya na isiyo na mikunjo.
9. Mayai na maini
Vyakula hivi huwa na wingi wa vitamini B na protini ambayo hutengenezwa kuwa seli za ngozi zinazokufa ili kuimarisha na kuboresha ngozi yako.
10. Maji
Maji huwa na molekyuli (molecules) ambazo husaidia shughuli za kiseli na huunganika katika seli za ngozi kuifanya laini na yenye mwonekano wa ngozi yenye afya. Ngozi iliyopungukiwa maji kupauka na kukosa mvuto. Hii huonekana zaidi mtu anapoishiwa maji mwilini na ngozi yake hupauka.
Usipende kutumia vipodozi vyenye kemikali kali ikiwemo mekyuri kwani utaharibu ngozi na kusababisha kansa ya ngozi kutokana na kemikali hizo. Na pia vipodozi hivyo vinaweza kuruhusu mionzi ya jua kuathiri ngozi yako.
Nivema kutumia vipododozi visivyo na kemikali kali huku ukuendelea kujipatia vyakula kama hivyo tulivyo viangalia. Hii itafanya ngozi yako kuwa nzuri zaidi na yenye afya.
Fuatana nami katika maada mbalimbali katika blog yangu au piga simu:
0752674467
0676674467
Jumamosi, 18 Februari 2017
Unajua namna ya kuzuwia meno kuoza?
Zuwia meno kuoza
Kuoza meno ni ugonjwa wa meno unaosababishwa na asidi inayozalishwa na bacteria wanaoishi mdomoni( normal flora). Asidi hii huondoa madini kama calcium ambayo huimarisha meno na mifupa.
Ili bacteria waweze kusababisha uzalishaji wa asidi kwa wingi inayoweza kupelekea meno kuoza, kinahitajika chakula cha sukari ambacho ndicho hubadilishwa na bacteria hao kuwa asidi inayopelekea meno kuoza.
Sio kila chakula cha sukali hupelekea meno kuoza, isipokua vyakula vya sukari vinavyo zalishwa viwandani (cariogenic foods) kama vile soda, pipi, chokleti, sukari nk.
Vyakula vya asili na vyenye sukari kama vile viazi vitam, ndizi mbivu, nanasi, muwa nk, haviwezi kusababisha meno kuoza.
Kwakadiri miaka inavoendelea na utandawazi kuongezeka ndivyo watu wanaachana na vyakula asili, hili hutoa jibu kwanini miaka ya sasa tatizo hili linaongezeka ukilinganisha na zamani.
Mambo yanayo pelekea meno kuoza
1. SukariMatumizi ya sukari Mara kwa mara husababisha uzarishwaji wa asidi kwa wingi inayopelekea meno kuoza.
Hoja sio uwingi wa sukari ila idadi ya matumizi kwa siku (frequency). Je, vyakula hivi hutumiwa marangapi kwa siku? ongezeko la matumizi huhatarisha meno kuoza hatakama unapiga mswaki.
2. Bacteria
Aina ya bacteria waliopo mdomoni na ukuaji wake (ongezeko lake) hupelekea ongezeko la uzalishaji wa asidi hatari kwa meno.
Bacteria huongezeka zaidi pale kinywa kinapo kuwa kichafu chenye mabaki mengi ya chakula ya muda mrefu ambayo hubadilishwa na kuwa ugaga(vitu vigumu vilivyo ganda juu ya meno). Vitu hivi hutengeneza makazi mazuri ya bacteria.
3. Meno yenyewe
Kuoza kwa meno hutegemeana na hali ya mwili ya mtu binafi kuweza kupambana dhidi ya tatizo. Hivyo wapo watu ambao kinga ya meno yao dhidi ya kuoza ni kubwa zaidi ya wengine.
4. Muda
Meno huchukua muda mrefu mpaka kufikia yanaoza ukayagundua, sio jambo la siku chache bali ni la miezi kadhaa hadi miaka.
Matokeo ya baadae ya kuoza meno
Jino kuuma au kuhisi ganzi linapopitiwa na vitu vya baridi na moto au vyenye sukari.kupoteza jino, jino kung'olewa endapo limelika sana au pale linaposababisha magonjwa mengine mdomoni.
Majipu ya mdomoni yanaweza kusababishwa na meno kuoza hasa pale bacteria wanapo pata nafasi ya maambukizi.
Maambukizi ya mfupa wa taya (ostemylitis), hili linaweza kupelekea kukatwa sehemu au kuondoa taya lote.
Kifo, mtu akipata magonjwa kama majipu makubwa, Kansa au maambukiza katika misuli ya usoni, anaweza kupoteza maisha.
Namna ya kuzuwia
Ili kuzuwia meno kuoza inapasa kupunguza utumiaji wa sukari mara kwa mara, utumiaji usizidi mara tatu kwa siku.Piga mswaki walau mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kabla ya kulala yaani baada ya chakula cha usiku. Jifunze namna ya kupiga mswaki kwa usahihi ili kuhakikisha kinywa chote kinawekwa safi.
Sukutua kinywa chako kila baada ya kutumia vyakula vya sukali vizalishwavyo viwandani kama vile pipi.
Epuka kulala usingizi na vyajula hivi mdomoni, hakikisha pia mtoto halali na vyakula hivi mdomoni.
Tembelea mara kwa mara kliniki ya meno walau mara mbili kwa mwaka ili kuchunguza kama kunadalili ya kuoza meno. Hili itakusaidia kujua na kukinga matatizo mengine ya kinywa na mano.
Tumia dawa ya meno wakati wa kupiga mswaki, hakikisha dawa unayotumiwa ina fluoride. Flouride husaidia kurudisha madini katika meno.
Nenda kliniki ya meno endapo una meno yaliyooza ili uyazibe kwa dawa yasindelee kuoza. Watu wengi kuenda kliniki baada ya maumivu jambo ambalo hupelekea jino kung'olewa.
Usikubali kupoteza jino lako hata moja kwani linakazi yake muhimu.
Fuatana nami katika blog yangu au piga simu:
+255752674467
+255676674467
Maada zinazo fanana
Afya ya uzazi na mahusiano
Afya ya mama na matoto
Afya ya mwili na akili nk
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






















